Pages

Sunday 27 April 2014

WORSHIP AFTERNOON SONG LYRICS


1.        BWANA NI MCHUNGAJI WANGU
Bwana ni mchungaji wangu,
Sitapungukiwa kitu,
Hunlaza penye majani mabi-i-chi,
Huniongoza kwenye maji matulivu.

Hunihuisha nafsi yangu,
Huniongoza kwa njia za haki,
Nipitapo bondeni mwamauti,
Sitaogopa wewe u nami.

Hakika wema nazo fadhili,
Zitanifuata mimi,
Nitakaa nyumbani mwa Bwana,
Siku zote za maisha yangu.

Gongo lako na fimbo yako,
Vinanifariji mimi
Waanda meza  mbele yaa-a-ngu
Machoni pa watesi wangu. ( To Chorus)

Nitakaa nyumbani mwa Bwana,
Siku zote za maisha yangu. (Mwisho)

2.        NASHUKURU BY MASELINAH
Umenipa uhai Baba, nafasi nyingine ya siku mpya,
Baba nashukuru-u-u,
Umeniponya roho na mwili, tabibu wa ajabu ewe Yesu,                       
Baba nashukuru-u-u,
Umeondoa laana baba, kabadilisha kuwa baraka
Baba nashukuru-u-u,
Kilio change ewe Yesu, kabadilisha kuwa furaha,
Baba nashukuru-u-u.
Kwa moyo wangu wote,
nasema asante kwako,
masiya nashukuru-u-u *2
Nilipokuwa mnyonge Baba, umekuwa nguvu yangu,
Baba nashukuru-u-u,
Nayo mishale ya yule mwovu, haijanipata umenilinda,
Baba nashukuru-u-u,
Umeniongoza Mwokozi wangu, kanisimamisha imara,
Baba nashukuru-u-u,
Umenitoa kwenye shimo la giza, kanileta kwenye mwanga,
Baba nashukuru-u-u,
(Chorus)*2

Yale yote umetenda, ni mengi mno,
                                        na yaajabu, sijui mimi nisemeje-ee
Yale Yahwe umenitendea, ni mengi mno,
                                        na yaajabu, sijui mimi nisemeje-ee
sijui mimi nisemeje-ee
(Chorus)
    Masiya nashukuru-u-u*3

3.        HERI SIKU MOJA MBELE ZAKO
Ewe Mungu wa majeshi,
Ninapenda kukaa nawe,
Maskani zako zapendeza,
Nazikondea kwa shauku kubwa

Heri siku moja mbele zako
Kuliko siku maelfu mbali na wewe,
E Bwana nguvu na msaada wangu,
nita-kupenda daima.

Moyo na mwili wangu Bwana,
Vya kulilia Mungu wangu,
Heri nikose vyote Baba,
Lakini nikupate wewe.

4.        SINA MUNGU MWENGINE
Sina Mungu mwengine,
Wakutegemea,
Mbinguni na duniani,
hapana mwengine,
sina cha kupendeza
wala cha faida
ila wewe Bwana wangu
Mungu wa milele

mwili na moyo wangu
vya weza zimia
bali Mungu ndiye nguvu za uhai wangu
yeye sehemu yangu
milele daima
nitaingia hema yake
Na sifa zake kuu

Ninani mwingine,
ajazaye roho yangu, na kunipa raha kamili
Ninani semeni,
akamboaye mwanadamu, na kumshindia shetani


5.        BABA NAOMBA BY KAHURA
Macho yangu, nayainuya,
Nibadilishe, Unibariki,
baraka zako, haina huzuni,
niza kudumu milele amina

Baba naomba, kubarikiwa nawe,
sitoki hapa usiponibariki *2

ukabadilisha, yakobo jina
ukamwita, isreael
maana yake, kubarikiwa
nami naomba kubarikiwa nawe.


Ninapokutazama utanininua,
Ninapokutazama utanibariki,
Ninapokutazama sitaogopa kamwe,
Sitoki hapa bila uguso wako.

Ukinigusa nimebarikiwa,
Uguso wako, ni baraka kwangu,
ulimgusa Batholomayo akaona,
Ndipo nasema, nataka uguso wako.

Sitoki hapa usinibariki.

6.        UNASTAHILI
Unastahili
unastahili
unastahili Bwana

(repeat)
Kupokea utukufu heshima na uweza
unastahili bwana

niwewe wastahili...
ni wewe wastahili bwana
(repeat)

7.        UNATAWALA MILELE by Chibalonza.
Solo: unatawala milele  (repeat)
Ubarikiwe milele (repeat)
Uinuliwe milele (repeat)

Milele milele Yesu ni mfalme
(Repeat)

Moyo wangu imba msifu mwokozi
(repeat).

8.        MWIMBIE BWANA
mwimbie bwana
msifu bwana
ametenda mambo ya ajabu(Echo)

Nitaimba wimbo mpya
Sifu Bwana wangu(Echo)

Sifu Bwana
Sifu Bwana
Sifu Bwana

Viumbe vyote
Sifu bwana

9.        HOW GREAT IS OUR GOD by Chris Tomlin.
The splendor of the king,
Clothed in majesty,
Let all the earth rejoice,
all the earth rejoice,

He wraps Himself in  light
and darkness tries to hide,
Trembles at His voice,
Trembles at His voice.


CHORUS.
How great is our God,
sing with me how great is our God
and all will see how great
how great is our GOD.

Age to age He stands
And time is in His hands
Beginning and the end
Beginning and the end

The God head three in one
Father Spirit Son
The lion and the lamb
The lion and the lamb


10.     USHIRIKA by Christine Shusho.
CHORUS.
Mimi  nataka ushirika nawe  ee.. ewe  roho
Mimi nataka ushirika nawe ee. …Roho *(repeat)
Nimekubali habari hizi, ya kuwa wewe ni Mungu  roho, roho nataka ushirika nawe
Ulikuwepo tokea mwanzo, ulishiriki kuniumba Nataka ushirika nawe
Nakuhitaji maishani unihifadhi moyo wangu roho ee roho wee nataka ushirika nawe
(Chorus)
Wayachukua maombi watuombea kwa kuugua roho,roho nataka ushirika nawe
Ukiwa nasi twatiwa, nguvu twafanya kazi kwa ujasiri roho, ee roho nataka ushirika nawe
Uyatawale maisha yangu sitaogopa nikiwa nawe eee roho
(Chorus)
Wewe Mungu uliye hai, tena roho wa kweli wewe kiongozi,nataka ushirika nawe
Wewe  mafuta ya shangwe tene harabuni yetu roho wa milele, nataka ushirika nawe
Wew roho msaidizi tena mshauri wetu wewe kidole cha Mungu nataka ushirika nawe…
(Chorus)

11.     UMETENDA MEMA by Kambua.
Nakushukuru wee, nakutukuza wee
Umenitendea mambo ya ajabu,
Mimi nisemeje,ili nikushukuru,
Nasema wewe Mungu,umenitendea.

CHORUS.
Umetenda mema,
umetenda mema,
umetenda mema,
ndio maana naimba. (repeat)

Wimbo wa moyo wangu, na nafsi yangu yote.
Yasema ewe Mungu umenitendea, Maisha yangu
Yote nakutolea wewe kwa maana ewe baba,
Umenitendea.

12.     HALLELUYAH.
Halleluyah
Halleluyah
Twalisifu jina lako tu.

wastahili sifa zote
umejivika nguvu
tamalaki mahali hapa
jina lako ni kuu.

Neema Yako yanitosha
Jioni asubuhi,mchana
Uwepo wako umenifunika
jina lako ni kuu.

Naja mbele zako kama nilivyo
Niwezeshe Bwana kukusifu
Naja mbele zako kama nilivyo
niwezeshe Bwana kukuabudu.


13.     HAIYE/YAHWEH
Nitamwimbia Bwana kwani yeye ni mwema
Yeye ni mwema x2

Yahweh x2
Hakuna muweza yote kama yeye

Yahweh x2
Dunia yote inamshangilia
Yahweh!!!

14.     SUBIRI USICHOKE                    
Usichoke, jitie moyo,
Bwana akujali,
Wakati wako utakapofika,
Hakuna atakayezuia baraka zako.

Macho yake yanazunguka,
Ulimwengu wote,
Kuonyesha nguvu zake,
kwa wale wamtumainio-o-o
Macho yake yanazunguka,
Ulimwengu wote,
Kuonyesha nguvu zake,
kwa wale wamtumainio.

Iteration (rudia mara kadhaa)
Subiri subiri wewe usichoke

15.     LET IT RAIN By Michael W. Smith

Let it rain,
Let it rain,

Open the flood gates of heaven,
Let it rain,
Let it rain.

16.     WEWE NI JEHOVAH- Faith mwangi
Ni Jehovah Rapha Mungu wetu wa uponya,
Magonjwa yote ameyaponya kwa damu yake
Ni Jehovah Rapha Mungu wetu wa uzima-a,
Wewe ni Mungu, wewe ni Bwana.

Chorus:
Wewe ni Jehova Mungu wetu wa uzima
Wewe ni Jehova Mungu wetu wa pekee
Mbingu na dunia zinakuabudu ewe mfalme
Wewe ni Mungu wewe ni Bwana

Ni Jehovah Jireh Mungu wetu anatujali
Mahitaji yetu anayajua yote-ee
Jehovah Jireh Mungu wetu atuhifadhi
Wewe ni Mungu, wewe ni Bwana
Chorus

Wewe ni Jehovah Ebenezer katufikisha
Hivyo mbali Mungu baba tumekuona
Wewe ni Jehovah Ebenezer katufikisha
Wewe ni Mungu, wewe ni Bwana
Chorus
Chorus(semi-tone up)*2No comments:

Post a Comment