Pages

Tuesday, 15 April 2014

Mawazo Kama Mbinu ya Ibilisi


Bwana wetu Yesu asifiwe. Naamini umezidi kuendelea vyema na kuchuchumilia ya mbinguni kwa hamu kubwa. Je, wawaza nini? Leo, nimeamua kuwaongelesha kwa lugha ya Kiswahili. Najihisi mwenye uzito mkuu moyoni na najiuliza, “Mbona mwanadamu asiweze kutambua maneno na matukio yaliyo bayana?” Hatuwezi kamwe kusema ni kukosa ufahamu bali tu nadhania ni kiburi kimeumbika ndani ya mioyo ya watu. Kila siku magazetini na kwa mtandao, kumejaa habari za maovu yanayoendelea hapa nchini na mataifa jirani na niyakushangaza mno.

Nataka kukuletea maelezo yatakayokuletea ufahamu wa haswa kinachotukula. Kila siku nashangaa kwa nini ni vigumu kukijua kinacho tuuma na ilihali kikaribu nasi yaani kati yetu. Sitakosa kurudia yakuwa maovu yanazidi kuongezeka na mwisho ukaribu. Bila kunukuu maandiko yoyote naamini kwamba ushawahi zisikia habari za mataifa ya Sodoma na Gomora. Mataifa haya  yalikuwa katika hali tuliyo hivi sasa  kabla ya kuharibiwa kwao. Laajabu ni jinsi tunaweza waona watu wale kuwa walipungukiwa na ufahamu bali tu wazembe sawia. Kwa nini twaitafuta gadhabu ya Mungu? Mungu in Mungu wa upendo, kweli, na vile vile ni yeye yule mtakatifu na atulipae kulingana na matendo yetu. Je wajua kuwa kwa ajili ya wingi wa upendo wa Mungu anatupatia muda wa kutosha wa kumtafuta  na kutengeneza urafiki naye? Labda hukujua hili. Hatujaangamizwa, ni kwa kuwa Mungu ametupa muda wa kubadili mienendo yetu.

Nataka kujadili chanzo kikuu cha ugumu  wa mioyo yetu. Mungu katupa ufahamu na mbinu kuu ziitwazo elimu. Elimu hii ilipasa iwe chanzo cha kumtumainia Mungu zaidi, lakini walimwengu wanatumia uvumbuzi huu kuenda kinyume na maagizo ya Mungu. Tumefika kiwango cha kuona twaweza endelea pasipo Mungu aliyetuumba. Fikira hizi ndio chanzo cha ndoa za watu wa jinsia moja, uchafu wa kila aina na hata kuwashurutisha wenzetu au kuwashirikisha katika mienendo yetu mibaya. Mbeleni nishawahi kusema kuwa vijinguo hivi vifupi na mitindo ya ajabu ndio chanzo cha fikira za ngono kila wakati kati ya wanaume. Nguo hizi pia zimebeba maroho yanayo wafanya kina dada hawatulii ndiyo maana si shida kwao kujihusisha kwa uchafu usio tajika. Picha na filamu chafu tunazozisambaza hasa kwa mtandao zaongezea mchango huo huo. Je kunaye atakayepona?

Ibilisi ameshabuni na tayari anatumia mbinu ya kutega mawazo. Kuna wale wanaofikiria kuwa haipaswi mtu yeyote kukashifu mienendo yao. Kwa mfano paparazzi mmoja nchini Tanzania alipowanasa mabinti wawili wakinyonyana ndimu alikaripiwa kwa kujulishwa angepatwa na janga iwapo picha hizo zingelifika magazetini. Ati dada hao wanadai ni kwa starehe zao na haipaswi kuwatatiza. Fikira hizi ndizo zitakazo tenga wengi na mapenzi ya Mungu. Nakuonya, matukio yanayo tendeka sasa ni kinyume na mapenzi ya wanadamu na Mungu. Kwani hujawai kusikia mara kwa mara watu wakidai kuwa jambo hili ni kinyume na tamaduni. Tamaduni ni za wanadamu na la Mungu ni sheria illiyoumbika kwa msingi wa utakatifu. Basi jua ya kwamba mawazo ya mwanadamu yameshatekwa nyara na ibilisi na ndiyo sababu ya matukio ya kuudhi ulimwenguni. Sikia haya: mama kufanya mapenzi na mwanawe, mwanamke mwenye mimba ya miezi nane kuzini juu ya bajaj, wanawake kujishirikisha kwa ngono hadharani (Uzinifu) mf bustani za kustarehe, vichakani, makaburini nk., watu kuzini kisha kutuma picha zao za utupu kwa mtandao, dada mtoto wa kiongozi wa kanisa aliyelelewa kwa kujulishwa habari za Mungu kukubali mwanamume kuramba nyeti yake!!! nk. Kunradhi kwa kuyataja haya, naona dhiki kuendelea na mifano hii ya vituko. Hizi ni baadhi ya habari za uchafu zinazosikisikitisha.

Najuwa bado wauliza ni vipi mawazo yaweza kamfanya mwanadamu kutenda haya. Mtoto mwenye umri mchanga yuajua pasipo kuambiwa na mtu ya kuwa yastahili kujifunika kwamba mtu asikaone sehemu za mwili zenginezo. Basi mwanamke au manamume aliyekomaa yampasa kuwa na hata kuelewa zaidi ya jambo hili. Kila tulitendalo huanza kwa wazo. Unapolipalilia kwa kulitafakari huzaa hisia na kiu ya kutaka kulitenda. Mwishoe tendo huibuka kulingana na ulivyo waza na kuwazua. Hebu basi tujiulize pamoja maswali haya baada ya ufahamu wa mawazo. Ni nini hasa kinacho mfanya mwanamke aliyekomaa kutafuta vazi linaloacha sehemu za mwili nje? Je, sababu ni fikira yakuwa hili ni jambo lisilostahili au kiburi cha moyo, ‘nalifanya vivyo hivyo iliihali halistahili.’ Kwa nini nisiwe na shauku ya jambo baya? Kwa nini hata nisimuogope Mungu aonaye hata kwa siri?

Mawazo yakitekwa na ibilisi humbadili mtu  na mawazo haya yatokao kwa ibilisi yaweza:
kukuza kiburi,
kutoa shauku ya kiungu,
kumfanya mtu kuwa mfungwa wa dhambi,
kukufanya kuishi maisha yasiyo kupasa uishi,
kukuzuia kupata ufahamu wa Mungu,
kukufanya kutumiwa vibaya na Ibilisi na mwishoe,
 kumuingiza mtu jehanamu mahali pa dhiki kuu milele.

Uchafu wote niliouataja hujatendeka mara moja tu, bali kila kukicha huyu naye kaonekana kafanya jambo lilo hilo. Basi ushajua shida ni mawazo. Yatupasa kumuomba Mungu mawazo yetu yasikaibwe. Sikiza hili, sote tunauwezo wakuyatenda wanayotenda marafiki zetu au mtu yeyote yule walakini twaweza jinasua kutoka kwayo. Mawazo yaliyofichika yakipona hata mtu kwa nje hupona. Haitahitajika kamwe kuhubiriwa tena kuhusu mavazi , mapambo na mienendo mibaya. Hatuwezi kwa akili zetu duni, twahitaji nguvu zaidi. Nguvu na njia ya pekee ni moja na ni Yesu. Usijipatie matumaini potevu. Hatuwezi kushinda katika misimamo ya maadili tu bali twahitaji mwongozo wa Roho Mtakatifu. Jehanamu na mbingu ni vya kweli na hakika. Jehanamu ilitengwa kwa ajili ya shetani na malaika zake waovu ilihali mbingu ni pa watoto wa Mungu aliye hai.  Mpe Yesu maisha yako na hutalemewa na tama za mwili. Mwili wapenda ulimwengu ni vilivyo ndani yake bali Roho atokaye kwa Baba hutufanya tupende yaliyo ya Mungu.

Naamini umenipata kwa njia safi kabisa. Niandikie ujumbe kwa barua pepe: goodnewsintlministries@gmail.comau piga simu 0710 333 072;  0710 333 081 iwapo wataka kujua zaidi kuhusu nyakati hizi au kumpa Yesu maisha yako ili atawale mawazo yako. Kumbuka kukiri na kutubu dhambi huleta kubadilishwa mawazo na kutiwa shauku ya Mungu na kumpata msaidizi atakaye kuongoza kwa njia ya haki.


No comments:

Post a Comment