Bwana wetu Yesu asifiwe. Naamini
umezidi kuendelea vyema na kuchuchumilia ya mbinguni kwa hamu kubwa. Je, wawaza
nini? Leo, nimeamua kuwaongelesha kwa lugha ya Kiswahili. Najihisi mwenye uzito mkuu
moyoni na najiuliza, “Mbona mwanadamu asiweze kutambua maneno na matukio yaliyo
bayana?” Hatuwezi kamwe kusema ni kukosa ufahamu bali tu nadhania ni kiburi
kimeumbika ndani ya mioyo ya watu. Kila siku magazetini na kwa mtandao, kumejaa
habari za maovu yanayoendelea hapa nchini na mataifa jirani na niyakushangaza
mno.
Nataka kukuletea maelezo yatakayokuletea ufahamu wa haswa
kinachotukula. Kila siku nashangaa kwa nini ni vigumu kukijua kinacho tuuma na
ilihali kikaribu nasi yaani kati yetu. Sitakosa kurudia yakuwa maovu yanazidi
kuongezeka na mwisho ukaribu. Bila kunukuu maandiko yoyote naamini kwamba
ushawahi zisikia habari za mataifa ya Sodoma na Gomora. Mataifa haya yalikuwa katika hali tuliyo hivi sasa kabla ya kuharibiwa kwao. Laajabu ni jinsi
tunaweza waona watu wale kuwa walipungukiwa na ufahamu bali tu wazembe sawia.
Kwa nini twaitafuta gadhabu ya Mungu? Mungu in Mungu wa upendo, kweli, na vile
vile ni yeye yule mtakatifu na atulipae kulingana na matendo yetu. Je wajua
kuwa kwa ajili ya wingi wa upendo wa Mungu anatupatia muda wa kutosha wa
kumtafuta na kutengeneza urafiki naye?
Labda hukujua hili. Hatujaangamizwa, ni kwa kuwa Mungu ametupa muda wa kubadili
mienendo yetu.
Nataka kujadili chanzo kikuu cha ugumu wa mioyo yetu. Mungu katupa ufahamu na mbinu
kuu ziitwazo elimu. Elimu hii ilipasa iwe chanzo cha kumtumainia Mungu zaidi,
lakini walimwengu wanatumia uvumbuzi huu kuenda kinyume na maagizo ya Mungu.
Tumefika kiwango cha kuona twaweza endelea pasipo Mungu aliyetuumba. Fikira
hizi ndio chanzo cha ndoa za watu wa jinsia moja, uchafu wa kila aina na hata
kuwashurutisha wenzetu au kuwashirikisha katika mienendo yetu mibaya. Mbeleni
nishawahi kusema kuwa vijinguo hivi vifupi na mitindo ya ajabu ndio chanzo cha
fikira za ngono kila wakati kati ya wanaume. Nguo hizi pia zimebeba maroho
yanayo wafanya kina dada hawatulii ndiyo maana si shida kwao kujihusisha kwa
uchafu usio tajika. Picha na filamu chafu tunazozisambaza hasa kwa mtandao
zaongezea mchango huo huo. Je kunaye atakayepona?
Ibilisi ameshabuni na tayari anatumia mbinu ya kutega
mawazo. Kuna wale wanaofikiria kuwa haipaswi mtu yeyote kukashifu mienendo yao.
Kwa mfano paparazzi mmoja nchini Tanzania alipowanasa mabinti wawili
wakinyonyana ndimu alikaripiwa kwa kujulishwa angepatwa na janga iwapo picha
hizo zingelifika magazetini. Ati dada hao wanadai ni kwa starehe zao na
haipaswi kuwatatiza. Fikira hizi ndizo zitakazo tenga wengi na mapenzi ya
Mungu. Nakuonya, matukio yanayo tendeka sasa ni kinyume na mapenzi ya wanadamu
na Mungu. Kwani hujawai kusikia mara kwa mara watu wakidai kuwa jambo hili ni
kinyume na tamaduni. Tamaduni ni za wanadamu na la Mungu ni sheria illiyoumbika
kwa msingi wa utakatifu. Basi jua ya kwamba mawazo ya mwanadamu yameshatekwa
nyara na ibilisi na ndiyo sababu ya matukio ya kuudhi ulimwenguni. Sikia haya:
mama kufanya mapenzi na mwanawe, mwanamke mwenye mimba ya miezi nane kuzini juu
ya bajaj, wanawake kujishirikisha kwa ngono hadharani (Uzinifu) mf bustani za
kustarehe, vichakani, makaburini nk., watu kuzini kisha kutuma picha zao za
utupu kwa mtandao, dada mtoto wa kiongozi wa kanisa aliyelelewa kwa kujulishwa
habari za Mungu kukubali mwanamume kuramba nyeti yake!!! nk. Kunradhi kwa
kuyataja haya, naona dhiki kuendelea na mifano hii ya vituko. Hizi ni baadhi ya
habari za uchafu zinazosikisikitisha.
Najuwa bado wauliza ni vipi mawazo yaweza kamfanya mwanadamu
kutenda haya. Mtoto mwenye umri mchanga yuajua pasipo kuambiwa na mtu ya kuwa
yastahili kujifunika kwamba mtu asikaone sehemu za mwili zenginezo. Basi
mwanamke au manamume aliyekomaa yampasa kuwa na hata kuelewa zaidi ya jambo
hili. Kila tulitendalo huanza kwa wazo. Unapolipalilia kwa kulitafakari huzaa
hisia na kiu ya kutaka kulitenda. Mwishoe tendo huibuka kulingana na ulivyo
waza na kuwazua. Hebu basi tujiulize pamoja maswali haya baada ya ufahamu wa
mawazo. Ni nini hasa kinacho mfanya mwanamke aliyekomaa kutafuta vazi
linaloacha sehemu za mwili nje? Je, sababu ni fikira yakuwa hili ni jambo
lisilostahili au kiburi cha moyo, ‘nalifanya vivyo hivyo iliihali halistahili.’
Kwa nini nisiwe na shauku ya jambo baya? Kwa nini hata nisimuogope Mungu aonaye
hata kwa siri?
Mawazo yakitekwa na ibilisi humbadili mtu na mawazo haya yatokao kwa ibilisi yaweza:
kukuza kiburi,
kutoa shauku ya kiungu,
kumfanya mtu kuwa mfungwa wa dhambi,
kukufanya kuishi maisha yasiyo kupasa uishi,
kukuzuia kupata ufahamu wa Mungu,
kukufanya kutumiwa vibaya na Ibilisi na mwishoe,
kumuingiza mtu
jehanamu mahali pa dhiki kuu milele.
Uchafu wote niliouataja hujatendeka mara moja tu, bali kila
kukicha huyu naye kaonekana kafanya jambo lilo hilo. Basi ushajua shida ni
mawazo. Yatupasa kumuomba Mungu mawazo yetu yasikaibwe. Sikiza hili, sote
tunauwezo wakuyatenda wanayotenda marafiki zetu au mtu yeyote yule walakini
twaweza jinasua kutoka kwayo. Mawazo yaliyofichika yakipona hata mtu kwa nje
hupona. Haitahitajika kamwe kuhubiriwa tena kuhusu mavazi , mapambo na mienendo
mibaya. Hatuwezi kwa akili zetu duni, twahitaji nguvu zaidi. Nguvu na njia ya
pekee ni moja na ni Yesu. Usijipatie matumaini potevu. Hatuwezi kushinda katika
misimamo ya maadili tu bali twahitaji mwongozo wa Roho Mtakatifu. Jehanamu na
mbingu ni vya kweli na hakika. Jehanamu ilitengwa kwa ajili ya shetani na malaika
zake waovu ilihali mbingu ni pa watoto wa Mungu aliye hai. Mpe Yesu maisha yako na hutalemewa na tama za
mwili. Mwili wapenda ulimwengu ni vilivyo ndani yake bali Roho atokaye kwa Baba
hutufanya tupende yaliyo ya Mungu.
Naamini umenipata kwa njia safi kabisa. Niandikie ujumbe kwa
barua pepe: goodnewsintlministries@gmail.comau piga simu 0710 333 072; 0710 333 081 iwapo wataka kujua zaidi kuhusu nyakati hizi au
kumpa Yesu maisha yako ili atawale mawazo yako. Kumbuka kukiri na kutubu dhambi
huleta kubadilishwa mawazo na kutiwa shauku ya Mungu na kumpata msaidizi
atakaye kuongoza kwa njia ya haki.
No comments:
Post a Comment